KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 17, 2011

Steve McClaren AJIONDOA KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA UMENEJA.


Aliekua kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Steve McClaren amekanusha taarifa za kuwa mbioni kuomba nafasi ya kuwa meneja wa klabu ya West Ham utd ambayo msimu ujao itashiriki ligi daraja la kwanza nchini humo.

Steve McClaren amekanusha taarifa hizo baada ya kuhusishwa na vyombo vya habari kwamba yu tayari kuiomba nafasi ya umeneja iliyoachwa wazi huko Upton Park na Avram Grant ambae alitimuliwa kazi saa chache mara baada ya mchezo wa ligi dhidi ya Wigan Atheltics mwishoni mwa juma lililopita.

McClaren, ambae nae ameshakumbwa na mkosi wa kutimuliwa kazi huko nchini Ujerumani wakati akikinoa kikosi cha Wolfsburg msimu huu ambapo kabla ya hapo alikua meneja wa FC Twente ya nchini Uholanzi amesema ni faraja kubwa sana kuona ni vipi mchango wake unavyohitajika katika soka la nyumbani kwao lakini kwa sasa hana budi kutuliza akili.

Mbali na kukiri huko pia akawatakia kila la kheri wale wote wanaoiwania nafasi ya umeneja ndani ya klabu ya West Ham utd yenye maskani yake makuu jijini London ambapo miongoni mwao yasemekana lipo jina la aliekua meneja wa Newcastle Utd Chris Hughton, meneja wa klabu ya QPR Neil Warnock, meneja wa klabu ya Swindon Town Gus Poyet pamoja na Sam Allardyce ambae alikua meneja wa Blackburn rovers.

Wakati huo huo mmiliki wa klabu ya West ham utd David Gold amesema hawana haraka ya kumteua meneja atakaekiongoza kikosi chao katika michuano ya ligi daraja la kwanza msimu ujao.

Amesema wanamuhitaji meneja mwenye sifa zinazokwenda sambamba na ligi hiyo pamoja na mwenye kujali uweledi wa kazi yake pindi atakapokua kazini hivyo itawachukua muda wa siku kadhaa kukamilisha utaratibu wa kumpata meneja mwenye vigezo wanavyovihitaji.

No comments:

Post a Comment