KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, May 25, 2011

Taye Ismaila Taïwo AFURAHIA USAJILI WAKE MILAN.


Beki wa pembeni wa kimataifa toka nchini Nigeria Taye Ismaila Taïwo amesema anaamini hatua ya kuihama klabu yake ya sasa ya Olympique de Marseille ya nchini Ufaransa na kujiunga na klabu bingwa nchini Italia AC Milan ni mafanikio makubwa katika maisha yake.

Taye Ismaila Taïwo mwenye umri wa miaka 26 amesema maisha yake ya soka yamekua mazuri toka alipoanza kucheza soka la kulipwa barani Ulaya mwaka 2005 akiwa na klabu ya Olympique de Marseille hivyo anastahili kutangaza hadharani kwamba bado anaendelea kupata mafanikio.

Beki huyo tayari ameshafanyiwa vipimo huko San Siro yalipo makao makuu ya klabu yake mpya ya AC Milan na amefanikiwa kupita katika vipimo hivyo ambapo hatua huyo imefanywa baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu huku akiondoka nchini ufaransa akiwa kama mchezaji huri.

Amesema haofii lolote juu ya kuanza maisha mapya nchini Italia zaidi ya kufurahia changamoto mpya ambazo amedai zitaendelea kumjenga katika harakati za kiushindani hasa ukizingatia umri wake unaruhusu changamoto mbali mbali za mchezo huo.

Amesema Ac Milan ni klabu kubwa na yenye hostoria ya kipekee duniani kama ilivyo kwa klabu kama Manchester United, Juventus, Chelsea, Arsenal pamoja na FC Barcelona na anajihisi mwenye furaha kutarajia kucheza na wachezaji kama Zlatan Ibrahimovic, Alexandre Pato pamoja na Clarence Seedorf.

No comments:

Post a Comment