KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, May 19, 2011

TUPO NYUMA YA ARSENE WENGER KWA 200%

Baada ya kumaliza msimu wa sita bila ya kuwa na taji la aina yoyote, mashabiki wa klabu ya Arsenal wametakiwa kuamini kwamba meneja wa klabu yao Arsene Wenger ana uwezo mkubwa wa kumaliza kiu inayowakabili msimu ujao.

Ufahamu huo kwa mashabiki wa klabu ya Arsenal umetoklewa na beki wa pembeni wa kimataifa toka nchini Ufaransa Bacary Sagna ambapo amesema Arsene Wenger bado anastahili kuaminiwa ndani ya klabu hiyo ya mjini London kufuatia uwezo wake mkubwa pamoja na mbinu ambazo siku za hivi karibuni zitazaa matunda ya mafanikio.

Sagna amesema wao kama wachezaji wapo nyuma ya meneja huyo wa kifaransa kwa asilimia 200 huku wakiamini msimu ujao kuna lolote linaweza kupatikana hivyo imani hiyo inatakiwa kuwavaa hadi mashabiki wa Arsenal ambao msimu huu wameendelea kuumizwa na matokeo mabovu.


katika hatua nyingine Bakari Sagna amezungumzia taarifa za kuhama kwa nahodha na kiungo wa klabu ay Arsenal Cesc Fabregas ambae anahusishwa na taarifa za kutaka kurejea nchini kwao Hispania kujiunga na moja ya klabu kubwa nchini humo.

Sagna amesema anaamini kiungo huyo atabaki klabuni hapo msimu ujao kufuatia mkataba wake aliosaini miaka miwili iliyopita na kutoonekana kwake uwanjani katika michezo mitatu iliyopita kunasababishwa na majeraha ya nyama za paja yanayomsumbua na si vinginevyo kama ivyoelelezwa katika vyombo mbali mbali vya habari.

Wakati huo huo meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger nae amezungumzia suala hilo linalomuhusu nahodha na kiungo wake Cesc Fabregas ambapo amesema bado anaamini mchezaji huyo ataendelea kuwepo huko Emirates kwa msimu ujao wa ligi.

Wenger amezungumzia suala hilo katika mkutano na waandishi wa habari uliolenga kuzungumzia mchezo wa mwishoni mwa juma hili ambapo Arsenal watakuwa ugenini kuwakabili Fulham huko Craven Cottage.

No comments:

Post a Comment