KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, May 28, 2011

TUPO VIZURI, NA MESSI ATAKABWA BILA SHAKA.


Beki wa pembeni wa klabu ya Man utd Patrice Evra amesema mchezo wa hii leo hawatouchukulia kama sehemu ya kutaka kulipiza kisasi cha kufungwa na Barcelona katika mchezo wa hatua ya fainali ya ligi ya mabingi barani ulaya katika msimu wa mwaka 2008-09.

Patrice Evra amesema mchezo wa hii leo wanauchukulia kama michezo mingine na watacheza kama ilivyo kawaida yao huku malengo makubwa ni kupata ushindi ambao utaebndelea kudhirisha ubora wa kikosi cha Man utd msimu huu.

Evra amekiri kwamba bado ubora wa kikosi chao upo pale pale na ubora wa Fc Barcelona utaendelea kuwa pale pale hivyo ni jukumu la kila mmoja wao kufanya jitihada binafsi ya kumchukua mwali wa ulaya usiku huu.

Katika hatua nyingine beki huyo akamzungumzia kiungo mshambuliaji wa klabu ya Barcelona Lionel Messi kwa kusema ni mchezaji wa kipekee ambae hawezi kukabwa na mtu mmoja kufuatia uchezaji wake wa kuhama hama anapokua uwanjani.

Evra pia akagusia suala la kucheza nyumbani usiku huu kwa kusema halipi kipaumbele sana, kwani katika mchezo wa hatua ya fainali y0a mwaka 2009 mashabiki wengi waliokuwepo Stadio Olimpico mjini Roma nchini Italia walikua ni wa Barcelona.

No comments:

Post a Comment