KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, May 30, 2011

Yohan Cabaye KUANZA MAISHA NCHINI UINGEREZA.


Kiungo wa nchini Ufaransa pamoja na klabu bingwa nchini humo Lille Yohan Cabaye, amekamilisha dili la kujiunga na klabu ya Newcastle Utd ambayo imejipanga kufanya kweli katika msimu ujao wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Taarifa zilizonukuliwa kutoka kwenye gazeti la michezo la kila siku la nchini Ufaransa liitwalo ya L'Equipe zimeeleza kwamba Yohan Cabaye amefanya maamuzi ya kujiunga na klabu hiyo ya St James Park kufuatia meneja wa klabu ya Lille Rudi Garcia kukubali kumuuza kwa kiasi cha Euro million tano.

Gazeti hilo limeendelea kubainisha kwamba maamuzi hayo yamefikiwa na meneja huyo kufautia Yohan Cabaye kutaka kuondoka klabuni hapo na kuelekea nchini Uingereza kujiunga na klabu ya Newcastle Utd ambayo amedai anaipenda huku akiamini kufanya hivyo ni sehemu ya kupata changamoto mpya katika soka lake.

Hata hivyo kuondoka kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 bado kutaendelea kukumbukwa na mashabiki wa soka nchini Ufaransa hususan wale wa klabu ya Lille kufuatia uwezo wake binafsi ambao ulichangia kwa kiasi kikubwa kuiwezesha klabu hiyo kutwaa taji la kwanza msimu huu toka mwaka 1954.

Yohan Cabaye bado alikua na mkataba na klabu ya Lille hadi mwaka 2013.

No comments:

Post a Comment