KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 31, 2011

Youssouf Mulumbu AJIWEKA PEMBENI.


Kiungo wa klabu ya West Bromwich Albion Youssouf Mulumbu amejiondoa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo ambacho kitarejea kwenye kampeni za kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya bara la Afrika za mwaka 2012 kwa kupambana na na Mauritius June 5.

Mtendaji mkuu wa timu ya taifa ya jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo Kamango Tsibola amesema Mulumbu alimfikishia taarifa hizo kupitia ujumbe mfupi wa simu ambao ulisomeka hatokuwepo kikosini kufutia sababu za majeraha yanayomkabili.

Kamango Tsibola amesema kiungo huyo alitarajiwa kuondoka mjini Paris nchini Ufaransa mwishoni mwa juma hili sambamba na wachezaji wengine wa jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo wanaosukuma soka la kulipwa barani Ulaya.

Wachezaji wengine wanaosukuma soka la kulipwa barani ulaya ambao hawatokuwepo katika kikosi cha jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo ni kiungo wa klabu ya SC Freiburg ya nchini Ujerumani Cedric Makiadi, ambae kwa sasa yupo katika fungate baada ya kufunga ndoa May 27.

Kutokuwepo kwa kiungo huyo kumetoa nafasi kwa kiungo wa DC Motema Pembe Kanu Mbiyavanga kuitwa kikosini.

Nae mshambuliaji wa klabu ya La Gantoise ya nchini Ubelgiji Mboyo Ilumbe nae hatokuwepo kikosini kufautai kuumia akiwa katika mchezo wa mwisho wa ligi ya nchini humo huku mshambuliaji wa klabu ya St Trond ya nchini Ubelgiji pia Mbuyi Mutombo akiwa bado hajafanya maamuzi ya kuichezea jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo ama Ubelgiji kutokana na kuwa na uraia wa nchi hizo mbili.

Katibu mkuu was shirikisho la soka la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo Ediba Bedi amesema nafasi ya Mulumbu, Ilumbe pamnoja na Mutombo hazitojazwa na wachezaji wengine katika kikosi hicho cha timu ya taifa.

No comments:

Post a Comment