KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, June 11, 2011

Alberto Aquilani NA NDOTO ZA KUTAKA KUBAKI NYUMBANI.


Wakala wa kiungo wa klabu ya Liverpool ambae msimu wa mwaka 2010-11 aliitumikia klabu ya Juventus kwa mkopo Alberto Aquilani amesema kuna dalili njema kwa kiungo huyo kubaki nchini humo kama matarajio yake alivyo yakusudia.

Franco Zavaglia wakala wa mchezaji huyo amesema amekua na mazungumza ya karibu na viongozi wa klabu ya Liverpool juu ya mustakabali wa mchezaji wake na jibu analolipata huko ni kutakiwa na subra licha ya kufahamika kwamba Alberto Aquilani analazimika kurejea Anfield mwezi July tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa ligi baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Juventus.

Franco Zavaglia pia amegusia suala la uwezekano wa kiungo huyo kusalia katika klabu ya Juventus ambapo amsema uwezekano huo ni mdogo sana kufuatia uongozi wa klabu hiyo kushindwa kuonyesha dalili za kutaka kuendelea nae msimu ujao.

Hata hivyo wakala huyo amesema endapo uongozi wa klabu ya Juventus utakuwa tayari kufanya hivyo bado yu tayari kuwakutanisha na viongozi wa klabu ya Liverpool ili waweze kumaliza dili la kumsajili moja kwa moja.

Katika hatua nyingine Franco Zavaglia amekanusha taarifa za Alberto Aquilani kuwa mbiono kujiunga na klabu ya Napoli ambayo msimu ujao itashiriki michuano ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ya nchini Italia.

Amesema hana taarifa zozote juu ya klabu ya Napoli kutaka kumsajili mchezaji huyo lakini pia akaaendelea kufungua milango kwa viongozi wa klabu hiyo ya Stadio San Paolo.

Wakati huo huo vyombo vya habaria nchini Italia vimekua vikiripoti kwamba Alberto Aquilani anawindwa kwa udi na uvumba na mabingwa wa soka nchini humo AC Milan.

No comments:

Post a Comment