KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, June 13, 2011

Alex McLeish AJIUZULU KWA NJIA YA BARUA PEPE.


Uongozi wa klabu ya Birmingham city umethibitisha kupokea barua pepe kutoka kwa meneja wa klabu hiyo Alex McLeish ambayo imeeleza hatua za kujiuzulu kwake kama meneja wa kikosi cha Blues.

Mwenyekiti wa klabu hiyo iliyoporomoka daraja katika msimu wa mwaka 2010-11 Peter Pannu amesema taarifa hizo kupitia njia ya barua pepe ziliwafikia jana na wao kama viongozi hawana hiyana na maamuzi yaliyochukuliwa na Alex McLeish .

Maamuzi ya meneja huyo wa kiscotish yamekuja ikiwa ni majuma kadhaa yamepita baada ya bodi ya uongozi wa klabu ya Birmingham city kukubaliana Alex McLeish aendelee na kibarua chake klabuni hapo licha ya kikosi chake kuporomoka daraja.

Matimaini makubwa ya bodi hiyo kufanya hivyo, ni imani iliyokuwepo dhidi ya Alex McLeish ambapo alipewa matarajio makubwa ya kukirejesha kikosi chake kwenye michuano ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza baada ya msimu mmoja.

Hata hivyo fununu zaeleza kwamba Alex McLeish huenda akawa na mipango ya kutaka kujiunga na mahasimu wakubwa wa Birmingham city, klabu ya Aston Villa ambao kwa sasa ipo kwenye mchakato wa kumsaka mrithi wa Gerard Houllier alieamua kujiweka pembeni kwa sababu za kiafya.

No comments:

Post a Comment