KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, June 1, 2011

Antonio Conte ARUDI NYUMBANI Stadio Olimpico di Torino.


Kiungo wa zamani wa klabu ya Juventus Antonio Conte ametajwa kuwa meneja wa klabu hiyo baada ya kutimuliwa kazi kwa Luigi Del Neri siku kadhaa zilizopita.

Antonio Conte ametajwa kuwa meneja wa klabu hiyo ya Stadio Olimpico di Torino baada ya kusiani mkataba wa miaka miwili ambao unaaminiwa utamuongoza katika shughuli zake za kila siku klabuni hapo na kutimiza mafanikio yanayohitajika.

Jukumu kubwa alilopewa Conte mwenye umri wa miaka 41, ni kuhakikisha anarejesha hadhi ya klabu hiyo yenye historia kubwa nchini Italia, baada ya kumaliza katika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi wa msimu wa mwaka 2010-11.

Antonio Conte anarejea klabuni hapo baada ya kutangaza kustahafu soka mwaka 2004 ambapo aliitumikia Juventus katika michezo 295 na kufunga mabao 29 huku akiwa miongoni mwa wachezaji walioiwezesha klabu hiyo kutwaa vikombe kadha wa kadha.

Msimu wa mwaka 2010-11 Antonio Conte alikinoa kikosi cha Siena ambacho kilimaliza kikiwa katika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi daraja la kwanza ya nchini Italia ambapo sasa kikosi cha klabu hiyo msimu ujao kitashiriki ligi kuu nchini humo.

No comments:

Post a Comment