KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, June 10, 2011

ASTON VILLA WAACHWA KWENYE MATAA, MCHANA KWEUPEEEEEEEEE.


Meneja wa klabu ya Wigan Athletic Roberto Martinez ameipiga chini ofa ya viongozi wa klabu ya Aston Villa na badala yake amejitia kitanzi cha kuendelea kukinoa kikosi chake ambacho kilinusurika kushuka daraja mwishoni mwa msimu wa mwaka 2010-11.

Roberto Martinez amefanya maamuzi hayo baada ya kupewa muda wa saa 24 na mwenyekiti wa klabu ya Wigan Dave Whelan hapo jana, ambae alikua tayari ameshampa uhuru wa kufanya anachokihitaji katika mawazo yake aidha kubaki klabuni hapo ama kuondoka na kujiunga na klabu ya Aston Villa.

Maamuzi yaliyofanywa na Roberto Martinez yamekwenda sambamba na hatua ya kusiani mkataba mpya ambao utaendelea kumuweka huko DW Stadium kwa kipindi kingine cha misimu kadhaa huku akiaminiwa kuleta mafanikio makubwa zaidi ya kukinusuru kikao chake kushuka daraja.

Taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa klabu hiyo ambayo imemnukuu meneja huyo wa kispaniola imeeleza kwamba kwa kipindi sasa amekua na mahusiano mazuri na mwenyekiti Wigan Dave Whelan na ameona si ustaarabu kumuacha solemba mzee huyo zaidi ya kuendelea kushirikiana nae.

Martinez, ambae pia alishawahi kuitumikiwa klabu ya Wigan Atheletic 1995–2001 pia amedai kwamba watu wa karibu na klabu hiyo pia wamekua chanzo cha kumrejesha katika mawazo chanya ya kuendelea kubaki klabuni hapo.

Klabu ya Aston Villa kwa sasa ipo kwenye mchakato wa kumsaka meneja wa kikosi chao kufuatia kuondoka kwa aliekua meneja klabuni hapo Garrard Houllier ambae ameamua kujiweka pembeni kwa lengo la kujipa muda wa kupumzika kutokana na hali yake ya kiafaya.

No comments:

Post a Comment