KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, June 6, 2011

Axel Thomas Witsel YU NJIANI KUELEKEA ITALIA.


Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka nchini humo, AC Milan wamethibitisha kuwa katika mazungumzo ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa pembeni wa klabu ya Standard Liege ya nchini ubelgiji Axel Thomas Witsel.

Makamu wa raisi wa klabu hiyo yenye maskani yake makuu huko San Siro Adriano Galliani amekieleza kituo cha televisheni cha Sky Sports cha nchini Italia kwamba wanamatarajio makubwa ya kumsajili mshambuliaji huyo ambae tayari ameonyesha nia ya kutaka kujiunga nao kwa ajili ya msimu ujao.

Adriano Galliani amesema mwishoni mwa msimu wa mwaka 2010-11 vilabu kadhaa toka barani Ulaya vilionyesha nia ya kutaka kumsajili Axel Thomas Witsel, lakini kwa bahati nzuri mshambuliaji huyo ameonyesha nia ya kutotaka kuelekea popote zaidi ya San Siro.

Makamu wa raisi wa klabu ya Standard Liege Luciano D'Onofrio amethibitisha kuwepo kwa mazungumzo hayo na amesema imani yake yamtuma watafikia muafaka wa kumuuza Axel Thomas Witsel kabla ya kuanza kwa msimu ujao.

Amesema baada ya kupokea ofa kutoka katika vilabu zaidi ya vitatu walifanya kikao na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 na amewathibitishia kuwa yu tayari kuelekea nchini Italia na si kwingine.

No comments:

Post a Comment