KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, June 3, 2011

BENT KUONGOZA SAFU YA USHAMBULIAJI KESHO.


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello amesema anaamini mshambuliaji wa klabu ya Aston Villa Darren Bent atakuwa mwiba mkali katika mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya utakaochezwa kesho katika uwanja wa Wembley dhidi ya Uswiz.

Fabio Capello ametangaza uaminifu kwa mshambuliaji huyo kufautia safu yake ya ushambuliaji hiyo kesho kumtegemea sana Darren Bent mwenye umri wa miaka 27 baada ya kuumia kwa Jermain Defoe huku Wayne Rooney akitumikia adhabu ya kuonyeshwa kadi ya njano.

Capello amesema anamfahamu vilivyo Darren Bent na mara kadhaa anapopata nafasi katika eneo la hatari huwa hapendi kuichezea hivyo anaamini ushindi utapatikana bila shaka mbele ya wapinzani wao hiyo kesho.

Hata hivyo amedai kwamba alikua na matarajio makubwa ya kumchezesha mshambuliaji huyo sambamba na Bobby Zamora ama Peter Crouch lakini anahofia afya za wachezaji hao ambazo zipo shakani.

Hofu kwa wachezaji hao wawili imeibuka baada ya kuumia wakiwa mazoezini ambapo Bobby Zamora anasumbuliwa na maumivu ya Hips na Peter Crouch anasumbuliwa na maumivu ya mgongo.

Kikosi kamili cha timu ya taifa ya Uingereza huenda kikaundwa wa wachezaji walioitwa na kocha mkuu Fabio Capello ambapo upande wa;

Makipa: Scott Carson, Joe Hart, Robert Green

Mabeki: Leighton Baines, Gary Cahill, Ashley Cole, Rio Ferdinand, Phil Jagielka, Glen Johnson, Joleon Lescott, John Terry, Kyle Walker

Viungo: Gareth Barry, Stewart Downing, Adam Johnson, Frank Lampard, James Milner, Scott Parker, Theo Walcott, Jack Wilshere, Ashley Young

Washambuliaji: Darren Bent, Peter Crouch, Bobby Zamora

No comments:

Post a Comment