KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, June 1, 2011

BIG SAM MENEJA MPYA WEST HAM UTD.


Hatimae uongozi wa klabu ya West Ham Utd umepata jibu la kitendawili cha kumsaka meneja wa klabu hiyo ambayo msimu ujao itashiriki katika ligi daraja la kwanza baada ya msimu wa mwaka 2010-11 kumalizika ikiwa mkiani mwa msimamo wa ligi kuu.

Uongozi wa West ham Utd umepata jibu la kitendawili hicho, kufuatia makubalo yaliyofikiwa kati yao na meneja wa zamani wa klabu za Bolton Wanderers, Newcastle utd pamoja na Blackburn Rovers Sam Alardyce.

Hatua hiyo imekamilishwa kufuatia kutimuliwa kazi kwa aliekua meneja wa klabu hiyo msimu wa mwaka 2010-11 Avram Grant, ambae alitupiwa virago baada ya kushindwa kufikia malengo ya kukibakisha kikosi chake katika michuano ya ligi kuu kwa ajili ya msimu jao wa ligi.

Mara baada ya taarifa kutangazwa hadharani meneja huyo mpya wa klabu ya West Ham Utd alihojiwa na vyombo vya habari na kukiri ni kweli ameafikiana na uongozi wa West Ham Utd na jukumu lake kubwa ni kuhakikisha wanarejea katika michuano ya ligi kuu misimu kadhaa ijayo.

Sam Alardyce mwenye umri wamiaka 56 amesema amelazimika kufanya maamuzi ya kurejea katika soka kwa utashi wake binafsi na kama West Ham Utd ingekua katika michuano ya ligi kuu asingefanya hivyo kwa sababu zake binafsi, lakini kuwepo katika ligi daraja la kwanza kumemvutia na anaamini hatua hiyo itadhihirisha utendaji wake wa kazi.

Wakati huo huo mshabiki wa klabu ya West Ham Utd wameonyesha kufurahishwa na ujio wa meneja huyo huku wengi wao wakiamini ugonjwa unaowasumbua umepata jibu la kurejea katika kiwango chao cha ushindani na pengine kuheshimika jijini landon na kwingineko.

No comments:

Post a Comment