KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, June 2, 2011

BLATTER AAHIDI KUFANYA KAZI KWA UWAZI NA UKWELI.


Baada ya kuchaguliwa kwa mara ya nne mfululizo kuwa raisi wa shirikisho la soka ulimwenguni kote FIFA Josep Sepp Blatter amesema shughuli iliopo mbele yake ni kuhakikisha soka linaendeshwa katika misingi ya uwazi na ukweli.

Blatter ambae alisalia pekee yake katika kinyang’anyiro cha kuwania uraisi wa FIFA mara baada ya kujiondoa kwa mpinzani wake Mohamed Bin Hammam mwishoni mwa juma lililopita amesema kila mmoja ulimwenguni anaguswa na mchezo wa soka na endapo watashindwa kufanya kazi kwa umoja huenda wakaharibikiwa.

Katika hatua nyingine mzee huyo wa umti wa miaka 75 ameahidi kufanya kazi na kila mmoja ulimwenguni na kuzika tofauti zilizojitokeza wakati wa kampeni za uombaji wa kura ambazo zilipelekea baadhi ya wajumbe kufungiwa na kamati ya maadili ya FIFA.

Katika uchaguzi wa FIFA uliofanyika jana huko mjini Zurich nchini Uswiz Josep Sepp Blatter alichaguliwa kwa kura 186 huku kura tatu zikimkataa.

No comments:

Post a Comment