KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, June 3, 2011

Brad Friedel AJIUNGA NA SPURS.


Klabu ya Tottenham Hotspur imefanikiwa kumsajili kwa uhamisho huru kipa wa klabu ya Aston Villa Brad Friedel.

Friedel, mwenye umri wa miaka 40, amekamilisha usajili huo baada ya mkataba wake na klabu ya Aston Villa kufikia kikomo mwishoni mwa msimu wa mwaka 2010-11 na alipotakiwa kusaini mkataba mpya aligoma kufanya hivyo.

Meneja wa klabu ya Tottenham Hotspurs Harry Redknapp mapema hii leo alithibitisha taarifa hizo kupitia mtandao wa klabu hiyo ya jijini London kwa kutamba kuwa amempata kipa mwenye uzoefu mkubwa ambae anaamini atakisaidia kikosi chake msimu ujao.

Kusajiliwa kwa Brad Friedel kunaashiria safari ya kipa wa kimataifa toka nchini Brazil Heurelho Gomes ambae amekua akifanya makosa ya kizembe anapokua langoni hatua mabyo ilipekea kuigharimu Spurs katika msimu wa mwaka 2010-11.

Brad Friedel tayari ameshacheza michezo 400 ya ligi kuu ya nchini Uingereza toka alipokwenda nchini humo mwaka 1997 na akiwa na klabu ya Aston Villa kwa kipindi cha miaka mitatu amecheza michezo 114.

Klabu nyingine alizozitumikia kipa huyo akiwa nchini Uingereza ni Liverpool pamoja na Blackburn Rovers.

No comments:

Post a Comment