KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, June 9, 2011

Bryan Robson AACHA KAZI NCHINI WA THAILAND.


Nahodha wa zamani wa klabu ya Man Utd pamoja na timu ya taifa ya Uingereza Bryan Robson amejiuzului nafasi yake ya kocha mkuu wa timu ya taifa ya Thailand.

Taarifa zilizotolewa na raisi wa shirikisho la soka nchini humo Worawi Makudi zimeeleza kwamba Bryan Robson amejiuzulu nafasi hiyo na wakati wowote kuanzia sasa nafasi yake itazibwa na kocha mwingine watakae mtangaza.

Worawi Makudi amesema Bryan Robson amefanya maamuzi ya kujiuzulu kwa sababu zake binafsi ambazo hakuwa tayari kuzianika hadharani, hatua ambayo inahisiwa huenda kulikua na mvurugano kati ya pende hizo mbili.

Hata hivyo toka Bryan Robson alipoanza kazi ya kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Thailand kumekua hakuna maendeleo yoyote zaidi ya nchi hiyo kuporomoka kwa nafasi 15 katika viwango vya soka ulimwenguni FIFA ambapo kwa sasa nchi hiyo inakamata nafasi ya 120.

Bryan Robson ambae tayari ameshavinoa vikosi vya klabu ya Middlesbrough, West Bromwich Albion, Sheffield United pamoja na Bradford City akiwa katika utawala wa kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Thailand alipatwa na matatizo ya kansa ya koo la kulazimika kufanyiwa matibabu.

No comments:

Post a Comment