KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, June 8, 2011

CAMEROON MAMBO MAGUMU KWELI KWELI !!


Jinamizi la matokeo mabovu bado linaendelea kuibana timu ya taifa ya Cameroon kufuatia matokeo ya sare yaliyopatikana katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Urusi uliochezwa usiku wa kumkia hii leo katika mji wa Salzburg nchini Austria.

Cameroon ambao wamepoteza matumaini ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika kwa mwaka 2012, wameshindwa kumaliza ukata wa kupachika mabao unaowaandama kwa muda sasa baada ya kubanwa vilivyo na wapinzani wao Urusi katika kipindi chote cha mchezo huo.

Hata hivyo beki wa timu ya raifa ya Cameroon Aurelien Chedjou almanusura aipatie bao timu hiyo katika dakika ya 79 baada ya kupiga kichwa mpira wa kona lakini umahiri wa kipa wa timu ya taifa ya urusi Vyacheslav Malafeev ulikatisha azma ya mchezaji huyo.

Nae mshambuliaji wa timu ya taifa ya Urusi Pavel Pogrebnyak alishindwa kuifungia timu hiyo bao dakika chache baadae kufuatia shuti lake kuokolewa vyema na kipa wa timu ya taifa ya Cameroon Guy N'dy Assembe.

Katika mchezo huo kocha mkuu wa timu ya taifa ya urusi Dick Advocaat hakumtumia mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Hotspurs Roman Pavlyuchenko, ambae mwishoni mwa juma lililopita alipachika mabao matatu pekee yake katika mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya dhidi ya Armenia.

Michezo mingine ya kimataifa ya kirafiki iliyochezwa usiku wa kumakia hii leo ni pamoja na:

Australia 0-0 Serbia
Austria 3-1 Latvia
Japan 0-0 Czech Republic
Norway 1-0 Lithuania
Rep of Ireland 2-0 Italy
South Korea 2-1 Ghana
Venezuela 0-3 Spain

No comments:

Post a Comment