KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, June 3, 2011

CAMEROONE, SENEGAL KUWAKOSA WACHEZAJI MUHIMU.Mshambuliaji wa klabu ya West Ham Utd ya nchini Uingereza Demba Ba, amejiondoka kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Senegal ambacho mwishoni mwa juma hili kitaendelea na kampeni za kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika za mwaka 2012.

Demba Ba aliefunga bao la ushindi katika mchezo uliopita dhidi ya Cameroon amejiondoa kikosini kufuatia maumivu ya nyonga aliyoyapata katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza ambapo West Ham Utd walichezea bakora tatu kwa sifuri dhidi ya Sunderland.

Habari zilizothibitishwa toka ndani ya timu ya taifa ya Senegal zimeeleza kwamba nafasi ya mshambuliaji huyo haitojazwa na mchezaji mwingine kufuatia muda mchache uliosalia kabla ya kuchezwa mchezo dhidi ya Cameroon huko mjini Yaounde siku ya Jumapili.


Kwa upande wa timu ya taifa ya Cameroon watamkosa kiungo wa klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza Alex Song ambae amelazimika kujiondoa kikosini kufuatia maumivu ya goti ambayo yanamsumbu.

Katika mchezo huo endapo Cameroon watakubali kupoteza, watajiweka katika mazingira magumu ya kucheza fainali zijazo za barani Afrika kufuatia hali kuwaendea kombo ambapo mpaka sasa wameshafikisha point 4 huku akitarajia kurejea uwanjani kwa mara ya nne.

Cameroon imepangwa katika kundi la tano lenye timu za Senegal wanaongoza kundi hilo kwa kuwa na point tisa, wakifuatiwa na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo wenye point 4 ambazo ni sawa na simba hao wasioshindika huku timu ya taifa ya Mauritius ikiburuza mkia kwa kutokuwa na point yoyote.

No comments:

Post a Comment