KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, June 2, 2011

Carles Puyol APIGWA KISU KWA MAFANIKIO.


Nahodha na beki wa klabu bingwa nchini Hispania pamoja na barani Ulaya kwa ujumla Carles Puyol amefanikiwa kufanyiwa upasuaji wa goti kwa hatua ya usalama wa salmini.
Carles Puyol mwenye umri wa miaka 33 amefanyiwa upasuaji huo chini ya madaktari wawili ambao ni Ricard Pruna pamoja na Ramon Cugat.

Daktari Ricard Pruna amesema kukamilika kwa hatua ya upasuaji wa goti kwa beki huyo ni furaha kwa kila mmoja ndani ya klabu ya Barcelona na itamchukua Carles Puyol muda wa miezi mitatu hadi minne kuwa nje ya uwanja.

Hatua hiyo inamfanya Carles Puyol kukosa sehemu ya michezo ya timu ya taifa ya Hispania ambayo kwa sasa ipo katika kampeni ya kutetea taji la barani Ulaya katika michezo ya hatua ya awali ambapo pia beki huyo atakosa sehemu ya mwanzoni mwa msimu ujao wa ligi.

No comments:

Post a Comment