KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, June 1, 2011

CARLOS TEVEZ ARUDISHWA KUNDINI.


Mshambuliwa klabu ya Man City Carlos Tevez hatimae ameitwa kwa mara ya kwanza katika timu ya taifa ya Argentina toka ulipoanza mwaka huu 2011.

Carlos Tevez ameitwa katika kikosi cha wachezaji 26 cha Argentina kwa lengo la kuanza maandalizi ya fainali za mataifa ya Amerika ya kusini *COPA AMERICA* zilizopangwa kufanyika nchini Argentina kuanzia July 1–July 24.

Kuitwa kwa mshambuliaji huyo mwenye umtri wa miaka 27 kunamaliza fununu zilizotawala huko nchini Argentina ambazo zilieleza kwamba Carlos Tevez hana nafasi ya kujumuishwa kikosini kufuatia kocha mkuu wa timu ya taifa Sergio Batista kuchoshwa na tabia zake za utovu wa nidhamu.

Fununu hizo ziliibuka kufuatia malumbano kati ya mshambuliaji huyo dhidi ya meneja wa klabu ya Man city Roberto Mancini ambae alichukizwa na kitendo Tevez cha kuondoka City Of Manchester na kurejea nyumbani bila kumuaga yoyote yule.

Kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kwa sasa kimewajumuisha wachezaji 26, lakini kocha mkuu wa timu hiyo Sergio Batista atalazimika kufanya mchujo na kusaliwa na wachezaji 22 ambao wanahitajika kwenye michuano ya Copa Amerika.

Kikosi kamili kilichoitwa kwa upande wa:

MAKIPA: Sergio Romero (AZ Alkmaar), Mariano Andujar (Catania), Juan Pablo Carrizo (River Plate)

MABEKI: Javier Zanetti (Inter Milan), Pablo Zabaleta (Manchester City), Nicolas Burdisso (AS Roma), Nicolas Pareja, Marcos Rojo (both Spartak Moscow), Gabriel Milito (Barcelona), Ezequiel Garay (Real Madrid), Luciano Monzon (Boca Juniors)

VIUNGO: Javier Mascherano (Barcelona), Esteban Cambiasso (Inter Milan), Ever Banega (Valencia), Fernando Gago, Angel Di Maria (both Real Madrid), Javier Pastore (Palermo), Diego Valeri (Lanus), Lucas Biglia (Anderlecht), Enzo Perez (Estudiantes)

WASHAMBULIAJI: Lionel Messi (Barcelona), Gonzalo Higuain (Real Madrid), Carlos Tevez (Manchester City), Diego Milito (Inter Milan), Sergio Aguero (Atletico Madrid), Ezequiel Lavezzi (Napoli)

No comments:

Post a Comment