KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, June 10, 2011

CHELSEA WACHIMBWA MKWARA MZITO.


Shirikisho la soka nchini humo limetishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya uongozi wa klabu ya Chelsea endapo utaendelea kumhadaa kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo Guus Hiddink.

Raisi wa shirikisho la soka nchini Uturuki Mahmut Ozgener ametangaza msimamo huku akiendelea kuwakumbusha viongozi wa klabu ya Chelsea kusahau kumpata Guus Hiddink ambae anafikiriwa kuwa mrithi wa Carlo Michelangelo Ancelotti alietimuliwa kazi humo Stamford Bridge mwishoni mwa mwezi uliopita.

Amesema kila mmoja ulimwenguni anatambu kwamba Guus Hiddink ana mkataba na shirikisho la soka nchini Uturuki kwa ajili ya kukinoa kikosi cha nchi hiyo kinachosaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Ulaya, hivyo wanaamini viongozi wa Chelsea wanafanya kusudi kumuhadaa kocha huyo wa kidachi.

Mahmut Ozgener amesema ushawishi wa viongozi wa klabu ya Chelsea kwa Guus Hiddink ulijidhihirisha wazi juma lililopita mara baada ya mchezo wa kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Ulaya ambapo Uturuki ilipata matokeo ya sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Ubelgiji ambapo vyombo vya habari vya nchini Uingereza vilianza kuripoti kwamba Uturuki hawana nafasi ya kusonga mbele hivyo The Blues wana uwezo wa kumpata kirahisi kocha huyo.

Hata hivyo tayati Guus Hiddink ameshakanusha taarifa za kuwa mbioni kujiunga na klabu yoyote kwa hivi sasa na badala yake mawazo na akili yake ameigeuzia katika timu ya taifa ya Uturuki.

No comments:

Post a Comment