KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, June 2, 2011

Darren Bent KUONGOZA KAMPENI YA KUPINGA USAJILI.Mshambuliji wa kimataifa toka nchini Uingereza Darren Bent ametoa ushawishi kwa wachezaji pamoja na mashabiki wa klabu ya Aston Villa kuhakikisha washambuliaji wa pembeni wa klabu hiyo Ashley Young pamoja Stewart Downing hawaondoki katika kipindi hiki cha usajili kwa ajili ya msimu mpya wa mwaka 2011-12.

Ushawishi huo kwa wachezaji pamoja na mashabiki umelazimika kutolewa na Darren Bent kufuatia kukiri kuwahusudu mno wachezaji hao wawili ambao amesema ngepnda kuwoana wanaendelea kubaki katika himaya ya Villa park.

Amesema ni kipindi kigumu kwa sasa kukubali kuwaachia wachezaji hao hasa ikizingatiwa wanahitaji kurejea katika makali kama ilivyokua siku za nyuma baada ya kufanya vibaya msimu wa mwaka 2010-11 ambao ulimalizika kwa Aston villa kushika nafasi ya 9 kwenye msimamo wa ligi.

Lakini pamoja na kuwepo kwa hatua hiyo ya ushawishi bado inahisiwa Ashley Young pamoja Stewart Downing huenda wakaondoka kufuatia meneja wa klabu ya Aston Villa Gerard Houllier kutangaza kukaa pembeni kwa ajili ya kujipa muda wa kupumzika kutokana na hali yake ya kiafya.

Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana kwenye kambi ya timu ya taifa ya Uingereza wachezaji hao wawili walionyesha hali ya kumuhusudu sana meneja huyo wa kifaransa huku wakijipa matumaini huenda angeendelea na utaratibu wa kukinoa kikosi cha The Villians.

Stewart Downing anahusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na klabu ya Liverpool kwa ada ya uhamisho wa paund million 18 huku Ashley young akihusishwa na taarifa za kuhitajika huko old Trafford yalipo makao makuu ya klabu bingwa nchini Uingereza .

No comments:

Post a Comment