KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, June 7, 2011

Didier Deschamps TUNAMUHESHIMU SANA - Jean-Claude Dassier.Raisi wa klabu ya Olympique de Marseille, Jean-Claude Dassier amekanusha taarifa za kuiondoka kwa meneja wa klabu hiyo Didier Deschamps.

Jean-Claude Dassier amekanusha taarifa hizo kufuatia vyombo mbali mbali vya habari nchini Ufaransa kuendelea kuzungumzia suala la kuondoka kwa meneja huyo ambae alikua nahodha wa kikosi cha timu ya taifa nchini hiyo kilichotwaa ubingwa wa dunia mwaka 1998.

Amesema Didier Deschamps mpaka sasa bado ana mkataba wa kuendelea kukinoa kikosi cha klabu hiyo yenye maskani yake makuu huko Stade VĂ©lodrome, mjini Marseille na wana uheshimu mkataba huyo.

Jean-Claude Dassier amebainisha kwamba mipango iliopo kwa sasa klabuni hapo ni kuhakikisha wanajipanga vyema kwa ajili ya msimu ujao wa ligi baada ya kushinbdwa kutetea ubingwa wa ligi daraja la kwanza katika msimu wa mwaka 2010-11 ambao ulishuhudia ubingwa ukielekea Stade Lille-Metropole, yalipo makao makuu ya klabu ya Lille.

No comments:

Post a Comment