KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, June 2, 2011

Dimitar Berbatov ATANGAZA VITA OLD TRAFFORD.


Mshambuliaji wa klabu bingwa nchini Uingereza Man Utd Dimitar Berbatov amesema atahakikisha anarejea katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo msimu ujao baada ya kusota benchi katika sehemu ya mwishoni mwa msimu wa mwaka 2010-11.

Dimitar Berbatov ametoa kauli hiyo ya changamoto kwa washambuliaji wenzake huko Old Trafford huku tayari akiwa anahusishwa na taarifa za kuwa mbioni kuuzwa na meneja wa klabu Sir Alex Ferguson ambae amekiri kuridhishwa na uwezo wa mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Mexico Havier Harnandez Balcazer Chicharito.

Akipohojiwa na kituo cha televisheni ya taifa cha nchini Bulgaria, Dimitar Berbatov amesema ni vigumu kukubaliana na hali halisi ya changamoto ndani ya kikosi cha klabu ya Man utd, lakini kwake anaamini hakuna kinachoshindikana hasa ikizingatiwa msimu wa mwaka 2010-11 alijitahidi na kufikisha idadi ya mabao 20 ambayo yamemuwezesha kuwa mfungaji bora sambamba na mshambuliaji wa klabu ya Man City Carlos Tevez.

Amesema jukumu kubwa alilonalo kwa sasa ni kujipanga vizuri na kuhakikisha anarudi vyema katika maandalizi yamsimu mpya wa ligi ambayo yataanza July 4, ambapo anaamini juhudi na uwezo wake binafsi utamvutia meneja Sir Alex Ferguson kumuingiza katika mipango ya kusaka taji la 20 la ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Hata hivyo tayari klabu kama Newcastle Utd ya nchini uingereza pamoja na Borussia Dortmund ya nchini Ujerumani zinahusishwa na taarifa za kutaka kutuma ofa ya kumsajili Dimitar Berbatov ambae pia inasemekana anapigiwa chepuo la kurejeshwa katika klabu yake ya zamani ya Tottenham Hotspurs ambayo ilimsajili mwaka 2006 akitokea Bayer Leverkusen.

1 comment:

  1. Wow, fantastic blog layout! Muda gani umekuwa mabalozi kwa? kufanya mabalozi kuangalia rahisi. Kuangalia jumla ya tovuti yako ni kubwa, kama vile maudhui!
    Custom Term Paper

    ReplyDelete