KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, June 6, 2011

FIFA NA MZOZO WA KUWTAUMIA MAMLUKI.


Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limetoa ruhusa kwa beki wa klabu ya Toulouse ya nchini Ufaransa Cheikh Mbengue kuichezea timu ya taifa ya Senegal baada ya kuthibitisha uraia wa mchezaji huyo.

FIFA wametoa ruhusa kwa mchezaji huyo kufuatia cheti chake cha kuzaliwa kuonyesha alizaliwa nchini Ufaransa lakini wazazi wake wawili wana asili ya nchini Senegal na tayari alikua ameshaitumikia timu ya taifa ya vijana ya Ufaransa.

Endapo ruhusa hiyo kutoka FIFA ingetolewa siku ya ijumaa ya juma lililopita kulikua na uwezekano mkubwa kwa Cheikh Mbengue kuichezea timu ya taifa ya Senegal ambayo ililazimishwa matokeo ya sare ya bila kufungana na timu ya taifa ya Cameroon siku ya jumamosi katika mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu fainali za mataifa ya bara la Afrika za mwaka 2012.

Katika hatua nyingine shirikisho la soka nchini Guinea, huenda likaingia katika matatizo makubwa na FIFA kufuatia kumujumuisha kikosini mchezaji Thierno Bah ambae ni raia wa nchini Uswiz mwenye asili ya nchini humo kwa ajili ya mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Madagascar.

Taarifa kutoka FIFA zimethibitisha kwamba uongozi wa shirikisho la soka nchini Guinea haukuwasilisha maombi yoyote ya kutaka mchezaji huyo aichezee timu ya taifa ya nchi hiyo kwa utaratibu maalum uliowekwa.

Nalo shirikisho la soka nchini Burkina Faso, huenda likaingia katika matatizo kama hayo endapo itathibitika walimtumia kipa Nilson mzaliwa wa nchini Brazil pamoja na beki Herve Zengue mzaliwa wa nchini Cameroon katika mchezo dhidi ya Namibia.

Wachezaji hao wawili waliitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Burkina Faso kufuatia asili yao kuwepo nchini humo.

No comments:

Post a Comment