KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, June 2, 2011

Gerard Houllier AKUBALIA KUJIWEKA PEMBENI.


Uongozi wa klabu ya Aston Villa umethibitisha taarifa za kuondoka kwa meneja wa klabu hiyo Gerard Houllier baada ya kuwa katika kibarua chake kwa muda wa miezi tisa iliyopiota.

Taarifa za kuondoka kwa meneja huyo wa nchini Ufaransa zimethibitishwa na mtendaji mkuu wa klabu ya Aston Villa Paul Faulkner ambapo amesema maamuzi ya Gerard Houllier daima watayaheshimu licha ya kuwaumiza kutokana na uwezo wake wa ufundishaji ulikua bado unahitajika klabuni hapo.

Amesema daima wataendelea kuwa nae katika kipindi hiki kigumu kufuatia matatizo ya kiafya ambayo yamepelekea kufikia maamuzi ya kuondoka huko Villa Park alipoelekea mwanzoni mwa msimu huu, mara baada ya kuondoka kwa Martin O’Neil.

Maamuzi yaliyofikiwa na Gerard Houllier yamechukua mkondo wake, kufuatia ushairi aliopewa na familia ambayo imemtaka kuwa pembeni kwa ajili ya kulinda heshima pamoja na afya yake ambapo kwa muda sasa amekua akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo.

Mshambuliaji wa klabu ya Aston Villa Daren bent amezungumzia masikitiko yake kufautia kuondoka kwa Gerard Houllier ambapo amesema ni vigumu kukubali lakini hakuna budi kufanya hivyo, na pia akamtakia kila la kheri.

No comments:

Post a Comment