KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, June 9, 2011

Gregorio Manzano ALAMBA KAZI Estadio Vicente Calderón.


Baada ya kuthibitisha hatua ya kuondoka kwa Enrique "Quique" Sánchez Flores, uongozi wa klabu ya Atletico Madrid umemtangaza Gregorio Manzano kuwa meneja wa kikosi cha klabu hiyo katika msimu wa mwaka 2011-12.

Gregorio Manzano mwenye umri wa miaka 55 anarejea klabuni hapo kwa mara ya pili baada ya wengi kuumbuka utawala wake katika msimu wa mwaka 2003-04 ambao ulishuhudia akikiongoza kikosi hadi katika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi.

Manzano amepewa jukumu la kukinoa kikosi cha klabu hiyo huku akiaminiwa anaweza kuleta mabadiliko makubwa hasa ikizingatiwa tayari ameshafanya mazuri akiwa na klabu ya Real Mallorca ambayo aliizawadia ubingwa wa kombe la mfalme mwaka 2003.

Msimu uliopita meneja huyo wa kimataifa toka nchini Hispania alikuwa na kikosi cha klabu ya Sevilla, na amefanikiwa kukiongoza hadi katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi ambapo sasa kinasubiri kushiriki michuano ya barani Ulaya msimu ujao.

Enrique "Quique" Sánchez Flores aliondoka huko Estadio Vicente Calderón, mwezi uliopita baada ya mkataba wake kufikia kikomo huku akiwa ameiongoza Atletico Madrid hadi katika nafasi ya saba katika msimamo wa ligi ya msimu wa mwaka 2010-11.

No comments:

Post a Comment