KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, June 11, 2011

Gregorio Manzano APIGA CHEPUO LA KWA MSHAMBULIAJI.Siku mbili baada ya kutangazwa kuwa meneja wa klabu ya Atletico Madrid Gregorio Manzano amesema mpaka sasa hakuna klabu yoyote iliyotuma ofa ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo pamoja na timu ya taifa ya Argentina Sergio Aguero ambae amewekwa sokoni toka mwezi uliopita.

Gregorio Manzano amesema suala hilo amelifahamu kwa undani baada ya kuzungumza na raisi wa klabu ya Atletico wa Madrid, Enrique Cerezo, mtendaji mkuu Gil Marin pamoja na mkurugenzi wa michezo Jose Caminero ambapo wote kwa pamoja wamemthibitishia hakuna kinachoendelea dhidi ya mshambuliaji huyo.

Meneja huyo amesema licha ya Sergio Aguero kuwekwa sokoni na uongozi bado ana mipango ya kumtumia msimu ujao ambapo anaamini endapo suala hilo litafanikiwa kuna kila dalili za sehemu ya mafanikio yake yakatimia.


Amesema mshambuliaji huyo siku zote amekua ni mwenye kujituma anapokua mazoezini na hata katika michezo ya kiushindani hali ambayo inamvutima na pia ameahidi kuketi sambamba na viongozi klabuni hapo kwa ajili ya kutazama namna ya kuahirisha mpango wa kumuuza katika kipindi hiki.

Sergio Aguero mwenye umri wa miaka 23 msimu uliopita alifanikiwa kupachika mabao 20 katika michezo yote ya ligi aliyocheza.

Hata hivyo tayari klabu kama Chelsea pamoja na Tottenham Hotspur zimeanza kuhusishwa na taarifa za kutaka kutuma ofa ya kumsajili mshambuliaji huyo kwa ajili ya msimu mpya wa ligi huku kigezo kikubwa kinachotarajiwa kutumiwa na vilabu hivyo ni kufuatia Atletico Madrid kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya barani Ulaya msimu ujao.

No comments:

Post a Comment