KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, June 9, 2011

HATUNA UWEZO WA KUMSAJILI FABREGAS !!


Mabingwa wa soka nchini humo pamoja na barani ulaya kwa ujumla FC Barcelona wamethibitisha kutokuwa na bajeti ya kutosha ambayo itawawezesha kumsajili nahodha na kiungo wa klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza Cesc Fabregas.

FC Barcelona wamethibitisha ufinyu wa bajeti yao kupitia kwa makamu wao wa raisi Javier Faus ambapo amesema kwa sasa wana kiasi cha paund million 40 ambacho hakiwezi kuendana na mipango ya kufanya usajili kwa wachezaji waliowadhamiria.

Amesema Arsenal wamemuweka sokoni Cesc Fabregas kwa ada ya uhamisho wa paund million 50 na hata kama watapunguza bado ada hiyo haiwezi kupungua zaidi ya paund million 40 hatua ambayo bado ni ngumu kwao.

Javier Faus pia amebainisha wazi kuwa mbali na Fabregas, wemepanga kumsajili mmoja kati ya wachezaji Alexis Sanchez, wa klabu ya Udanise ya nchini Italia ama Giuseppe Rossi wa klabu ya Villarreal ya nchini Hispania ambapo hatua hiyo amesema inaendelea kwabana.

Hata hivyo ameongeza kwamba endapo watahitaji bajeti yao iongezeke ni lazima wakamilisha utaratibu wa kuwauza wachezaji kama Bojan, Thiago Alcantara pamoja na Jeffren ambao wamewekwa pembeni katika mipango ya Josep Pep Guardiola Isala.

No comments:

Post a Comment