KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, June 11, 2011

JAMAA KADHAMIRIA KURUDI NYUMBANI.


Beki wa klabu ya Manchester City Jerome Boateng amejitoa muhanga kwa kueleza yu tayari kurejea nyumbani kwa ajili ya kujiunga na klabu ya Bayern Munich ambayo ina mpango wa kutaka kumsajili katika kipindi hiki.

Jerome Boateng ambae bado ana mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo ya mjini Manchester ameeleza wazi kiu yake ya kutaka kurejea nyumbani alipokua kwenye hafla maalum ya watu muhimu huko mjini Humburg baada ya kuhojiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Amesema tayari ameshamueleza meneja wa klabu ya Man city Roberto Mancini kuhusiana na msimamo huo na anaamini kila jambo litakwenda kama lilivyopangwa katika utaratibu wake wa kujiunga na klabu ya Bayern munich.

Amesema anaipenda na kuithamini klabu ya Man city lakini hana budi kutimiza dhamira yake ya kuondoka katika kipindi hiki baada ya kusaidiana na wengine huko City Of Manchester kutwaa ubingwa wa kombe la FA hatua ambayo imefanya klabu hiyo kutwaa taji lake la kwanza toka mwaka 1976.

Uongozi wa klabu ya Bayern Munich ukiongozwa na raisi wake Uli Honnes tayari umeshatangaza kuhamishia nguvu zake katika usajili wa Jerome Boateng baada ya kukamilisha usajili wa Manuel Neuer, Márcio Rafael Ferreira de Souza, pamoja na Nils Petersen wote kutoka kwenye klabu ya Schalke 04.

No comments:

Post a Comment