KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, June 13, 2011

JAMAA KAREJEA KATIKA UTAWALA WA SOKA.


Aliekuwa meneja wa klabu ay Wolfburg ya nchini Ujerumani Steve McClaren amefanikiwa kurejea katika soka la nchi hiyo kufuatai hii leo kutangazwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Nottingham Forest inayoshiriki ligi daraja la kwanza.

Steve McClaren ametangazwa kushika nafasi hiyo baada ya uongozi wa klabu ya Nottingham Foresh kumtimua kazi aliekua meneja wa klabu hiyo Billy Davies usiku wa kuamkia hii leo.

Steve McClaren anarejea katika utawala wa soka nchini Uingereza baada ya miezi minne ambayo ilishuhudia akitimuliwa kazi huko nchini Ujerumani kufuatia mambo kumendea kombo katika klabu ya Wolfsburg ambayo ilikua katika hatari hati ya kuporomoka daraja.

Hata hivyo inaaminiwa kwamba meneja huyo mwenye umri wa miaka 50 atakuwa na kila sababu ya kuipandisha daraja klabu ya Nottingham Forest ambayo msimu wa mwaka 2010-11 ilikosa nafasi hiyo baada ya kuondoshwa katika hatua ya michezo ya mtoano.

Mashabiki kadhaa wa klabu hiyo ya City Ground nao wameonyesha kuridhishwa na uteuzi wa Steve McClaren ambapo kwa nyakati tofauti walisikika wakisema uzoefu wa meneja huyo huenda ukakisaidia kikosi chao kufanya vyema msimu ujao na kufikia malengo ya kurejea katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza ambayo kwa mara ya mwisho walishiri kwenye msimu wa mwaka 1993-94.

Mbali na kutangazwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Nottingham Forest, McClaren bado alikua na nafasi ya kurejea katika utawala wa soka nchini Uingereza kufautia jina lake kujitokeza kwenye orodha ya mameneja ambao walikua wakifikiriwa kushika nafasi ya Roberto Martinez endapo angefanya maamuzi ya kujiunga na klabu ya Aston Villa mwishoni mwa juma lililopita.

No comments:

Post a Comment