KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, June 8, 2011

Jordan Henderson AENDA ANFIELD, David Ngog AENDA Stadium of Light.


Majogoo wa jiji Liverpool wamekubali kumsajili kiungo wa klabu ya Sunderland Jordan Henderson, baada ya kukamilika kwa mazungumzo ya pande hizo mbili mapema hii leo.

Liverpool wamekubali kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20 kwa ada ya uhamisho wa paund million 20 sambamba na makubaliano ya kumtoa mshambuliaji wa kifaransa David Ngog ambae anaelekea huko Stadium of Light.

Baada ya makubaliano kufikiwa Jordan Henderson alitarajiwa kuelekea mjini Liverpool kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya yake kabla ya kukamilisha taratibu zote za kuvaa jezi ya THE REDS msimu ujao.

Kusajiliwa kwa kiungo huyo huko Anfield ni sehemu ya mikakati iliyowekwa na meneja wa klabu ya Liverpool King Kenny Dalglish ambae amepania kurejesha heshima ndani ya klabu hiyo ambayo imepotea kwa misimu kadhaa sasa.

King Kenny Dalglish tayari ameshaonyesha muelekea wa kukiweka sawa kikosi chake kwa kufanya usajili wa washambuliaji mwezi januari mwaka huu ambapo alimsajili mshambuliaji kutoka nchini Uingereza Andy Carroll pamoja na mshambuliaji kutoka nchini Uruguay Luis Suarez ambao wameonyesha uwezo mkubwa wa kuisaidia Liverpool katika msimu wa mwaka 2010-11.

No comments:

Post a Comment