KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, June 10, 2011

KAKA ATANGAZA KUSUDIO LAKE.


Kiungo wa kimataifa toka nchini Brazil Ricardo Izecson dos Santos Leite Kaka amesema bado ana mapenzi ya dhati na klabu yake ya sasa na katu hapendezwi na taarifa zinazomuhusisha kuihama Real Madruid katika kipindi hiki.

Ricardo Izecson dos Santos Leite Kaka ambae yupo nyumbani kwao Brazil kwa mapumziko mara baada ya kuamlizika kwa amsimu wa mwka 2010-11 amesema jukumu lake kubwa ni kuhakikisha Anaitumikia kwa moyo mmoja klabu hiyo kwa ajili ya kulipa fadhila kwa uongozi pamoja na mashabiki ambao walimpokea akitokea AC Milan ya nchini Italia mwaka 2009.

Amesema wakati huu ni mgumu sana kwake kufuatia taarifa kadhaa kutolewa na vyombo vya habari juu ya kutaka kuondoka kwenye klabu hiyo ya Estadio Stantiago Bernabeu, lakini hana budi kuzipuuza taarifa hizo na kutazama mbele kwa ajilo ya kutimiza malengo aliyojiwekea.

Kaka mwenye umri wa miaka 29 amebainisha wazi kwamba kwa muda wa misimu miwili aliyokaa klabuni hapo amekua katika mazingira magumu ya kucheza soka lake la kawaida kufuatia majeraha kumuandama kila wakati hivyo anaona msimu ujao utaanza vizuri kwake na atacheza kwa kujituma kama ilivyo kwa wachezaji wengine.

Kaka alisajiliwa na Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa Euro million 68.5 ambayo imemfanya kuwa mchezaji ghali anaeshika nafasi ya pili duniani baada ya Cristiano Ronaldo.

No comments:

Post a Comment