KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, June 7, 2011

KATU HATUTORUDI NYUMA - Joseph Sepp Blatter


Raisi wa shirikisho la soka ulimwenguni FIFA Joseph Sepp Blatter amesema kamwe hatofufua zogo la tuhuma za rushwa zinazodaiwa kutawala katika utaratibu wa kuichagua nchi ya Qatar kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2022.

Joseph Sepp Blatter amesema kwa sasa hakuna umuhimu wa kuliibua suala hilo kufuatia mikakatia aliyoiweka ya kuhakikisha soka linasonga mbele na kutoa migogoro ya kunyoosheana vidole kwa makosa yaliyofanyika siku za nyuma.

Amesema pamoja na yeye binafsi kutokutaka kurejea zogo hilo, bado hawezi kuzuia shughuli ya kamati ya maadili endapo itataka kuliibua zogo hilo kwa lengo la kusafisha uozo unaowakabili baadhi ya wajumbe wa FIFA wanaodaiwa kuhusika katika suala la kutoa na kupokea mlungula.

Taarifa za siku kadhaa zilizopita zilidai kwamba wajumbe wawili kutoka barani Afrika ambao ni raisi wa CAF Issa Hayatou pamoja na Jacques Anouma wa nchini Ivory Coast walipokea mlungula wa dola za kimarekani million 1.5 [£916,000] ili waipigie kura Qatar.

Pia inadaiwa kwamba raisi wa shirikisho la soka barani Asia ambae ni raia wa Qatar Mohamed Bin Hammam alishiriki katika harakati za kuwanunua wajumbe wengine ili kuiwezesha nchi yake kuwa mwenyeji.

No comments:

Post a Comment