KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, June 3, 2011

Luis Enrique AFIKIRIWA STADIO OLYMPICO MJINI ROMA.


Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania pamoja na klabu ya Barcelona ambae kwa sasa ni kocha wa kikosi cha Barcelona B, Luis Enrique Martínez García, ameripotiwa kuwa mbioni kujiunga na klabu ya AS Roma.

Luis Enrique Martínez García ameripotiwa kuwa katika mipango hiyo kupitia taarifa zilizotolewa kwenye kituo cha televisheni cha Sky Sports cha nchini Italia ambapo zimeeleza kwamba uongozi wa klabu ya AS Roma umejinasibu kuwa tayari kumlipa Euro milion 1.6 kwa mwaka kama mshahara wake.

Pia taarifa hizo zimesisitiza kuwa mpango wa kumpeleka Luis Enrique Martínez García huko nchini Italia unamuhusishwa na mchezaji mwenzake wa zamani wa klabu ya Barcelona Ivan de la Pena ambae atakua msaidizi wake.

Luis Enrique mwenye umri wa miaka 41 amekua katika shughuli za kukinoa kikosi cha Barcelona B toka mwaka 2008 baada ya Josep Pep Guardiola Isala kusaini mkataba wa kukinoa kikosi cha wakubwa cha klabu hiyo huko Camp Nou.

AS Roma wanasaka meneja katika kipindi hiki baada ya aliekua meneja wa klabu hiyo Claudio Ranieri kuachia ngazi mapema mwaka huu kwa sababu za kutokuheshimiwa na baadhi ya wachezaji klabuni hapo, hatua ambayo ilipelekea uongozi wa klabu hiyo kumpa mkataba wa muda Vincenzo Montella.

No comments:

Post a Comment