KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, June 9, 2011

Luis Enrique Martínez García ALAMBA KAZI AS ROMA.


Kocha wa kikosi cha Barcelona B Luis Enrique Martínez García amekubalia kujiunga na klabu ya AS Roma ya nchini Italia baada ya kutakiwa kufanya hivyo majuma mawili yaliyopita.

Luis Enrique Martínez García amekubali kujiunga na klabu hiyo baada ya kuketi sambamba na viongozi wa AS Roma na kubaliana masuala la kimaslahi pindi atakapokua huko Stadio Ulimpico.

Sehemu ya makubaliano hayo yaliyofikiwa na pande hizo mbili ni kubadilishwa kwa benchi zima la ufundi ambapo sasa litakua chini ya mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Barcelona ambae atasaidiana na mchezaji mwenzake waliocheza wote huko Camp Nou Ivan De La Pena.


As Roma kwa kipindi cha miezi sita ya msimu wa mwaka 2010-11 walikua chini ya meneja wa muda Vincenzo Montella ambae aliombwa na uongozi kuliongoza benchi la ufundi kufuatia kuondoka kwa alikua meneja wa klabu hiyo Claudio Ranieri.

No comments:

Post a Comment