KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, June 9, 2011

MAN UTD WAGEUZA MACHO YAO ARSENAL KWA 100%.


Mabingwa wa soka nchini Uingereza Man Utd, wamebadili muelekeo wa kufanya usajili wa mchezaji anaecheza nafasi ya kiungo baada ya uongozi wa klabu ya Tottenham Hotspurs kuweka ngumu ya kumuuza Luka Modric.

Man utd wamebadili msimamo huo kwa kuelekeza macho yao kwa kiungo wa kimataifa kutoka nchini Ufaransa pamoja na klabu ya Arsenal Samir Nasri ambae amekua akihusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa huko Old Trafford.

Man Utd wamepata nguvu ya kubadili muelekeo huo kufautia Samir Nasri kuendelea na mpango wake wa kutotaka kusaini mkataba mpya na uongozi wa klabu ya Arsenal ili hali mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kufikia kikomo mwishoni mwa msimu ujao.

Hata hivyo bado haijaeleweka kama Samir Nasri atabadili msimamo huo kufuatia uongozi wa klabu ya Arsenal kumbembeleza kila kukicha ili akamilishe utaratibu wa kusaini mkataba mpya na kuondokana na taarifa za kujiunga na klabu ya Man utd.

Katika hatua nyingine Man utd wameendelea kuhusishwa na taarifa za kutaka kumsajili kiungo wa kimataifa kutoka nchini Uholanzi pamoja na klabu bingwa duniani Inter Milan Wesley Sneijder.

Man Utd wameendelea kuwepo katika mpango huo huku klabu ya Chelsea ikiingia katika utaratibu wa kuiwania saini ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27.

Tayari kibopa wa chelsea Roman Abramovich ameshatenga kiasi cha paund million 30 kwa ajili ya usajili wa Wesley Sneijder ambae msimu uliopita ada yake ya uhamisho ilitangazwa na uongozi wa klabu ya Inter Milan kuwa ni paund million 13.

No comments:

Post a Comment