KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, June 6, 2011

MCHAKATO WA KUFUZU FAINALI ZA MATAIFA YA AFRIKA 2012.


Mabingwa watetezi wa fainali za mataifa ya bara la Afrika timu ya taifa ya Misri wameendelea kujiwekea mazingira magumu ya kutetea ubingwa wao baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na timu ya taifa ya Afrika kusini.

Mabingwa hao wamelazimishwa matokeo hayo katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Afrika za mwaka 2012, uliochezwa mjini Cairo jana jioni ambapo mashabiki wengi wa nchini Misri waliamini huenda kikosi chao kingejipapatua na kupata ushindi.

Matokeo hayo ya bila kufungana yanaifanya timu ya taifa ya Misri kuendelea kuburuza mkia wa kundi G kwa kuwa na point mbili huku Afrika kusini wakiongoza kundi hilo kwa kufikisha point 8 wakifuatiwa na timu ya taifa ya Niger yenye point 6 na timu ya taifa ya Sierra Leone inakamata nafasi ya tatu kwa kuwa na point tano.

Mchezo mwingine wa kundi hilo ulikua kati ya timu ya taifa ya Niger dhidi ya Sierra Leone ambao walikubali kupoteza ugenini kwa idadi ya bao moja kwa sifuri.

Matokeo ya michezo mingine ya kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Afrika mwaka 2012 iliyochezwa jana ni pamoja na;

Group E: Mauritius 1-2 DR Congo.
Group C: Comoros 1-1 Libya.
Group K: Botswana 0-0 Malawi.
Group A: Zimbabwe 2-1 Mali.
Group B: Ethiopia 2-2 Nigeria.
Group H: Benin 2-6 Ivory Coast.
Group I: Swaziland 1-2 Sudan.
Group H: Burundi 3-1 Rwanda.
Group D: Afrika ya Kati 2-1 Tanzania.
Group J: Angola 1-0 Kenya.
Group A: Liberia 1-0 Cape Verde.
Group K: Tunisia 2-0 Chad

No comments:

Post a Comment