KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, June 6, 2011

Miroslav Josef Klose AFUNGULIWA MILANGO HUKO ALLIANZE ARENA.


Hatimae mazungumzo kati ya uongozi wa klabu ya Bayern Munich pamoja na mshambuliaji wa klabu hiyo Miroslav Josef Klose ya kuboresha mkataba, yamevunjika rasmi baada ya pande hizo mbili kushindwa kufikia muafaka.

Taarifa iliyotolewa katika mtandao wa klabu hiyo yenye maskani yake makuu huko Allianze Arena zimethibitisha kwamba mshambuliaji huyo sasa yu huru kuondoka na kujiunga na klabu yoyote ulimwenguni katika kipindi hiki.

Taarifa hizo imesisitiza kwamba mkataba rasmi wa Miroslav Klose unafikia kikomo June 30, mwaka huu hivyo uongozi wa Bayern hauna kinyongo dhidi yake zaidi ya kumtakia kila la kheri huko aendapo.

Sababu kubwa ya mazungumzo ya pande hizo mbili kuvunjia, ni mvutano uliokuwepo ambapo uongozi wa Bayern Munich ulitaka kumpa mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuwepo klabuni hapo, hatua ambayo imepingwa vikali na Miroslav Klose ambae amekua akihitajin kuongezwa mkataba wa miaka miwili.

Katika mazungumzo hayo upande wa uongozi uliwasilishwa na mwenyekiti Karl-Heinz Rummenigge ambae siku za mwanzo aliwathibitishia waandishi wa habari kufikiwa kwa muafaka licha ya mvutano uliokuwepo.

Miroslav Klose mwenye umri wa miaka 32 anaondoka Allianze Arena baada ya kuwepo huko kwa muda wa miaka minne na hii ni kuanzia mwaka 2007-11 ambapo alishuhudiwa akicheza michezo 98 na kupachika mabao 24.

Tayari klabu kama Trabzonspor ya nchini Uturuki, Valencia ya nchini Hispania pamoja na baadhi ya vilabu vya nchini Uingereza vinahusishwa na taarifa ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo mwenye rikodi ya kipekee ya upachikaji mabao katika timu ya taifa ya Ujerumani ambapo mpaka sasa ameshapachika mabao 61 katika michezo 109 aliyocheza.

Wakati Miroslav Klose akionyeshwa mlango wa kutokea huko Allianze Arena, Bayer Munich wana matumaini makubwa ya kumsajili beki wa kimataifa toka nchini Ujerumani pamoja na klabu ya Manchester City Jerome Boateng.

Jerome Boateng beki anaecheza nafasi ya pembeni anapigiwa upatu wa kurejea nyumbani huku uongozi wa klabu ya Man City ukiwa tayari umeshatangaza dau la paund million 10.5 kama ada ya uhamisho wake.

Tayari Bayern Munich wameshafanikiwa kumsajili kipa Manuel Neuer, beki wa pembeni Márcio Rafael Ferreira de Souza pamoja na mshambulaiji Nils Petersen wote kutoka kwenye klabu ya Schalke 04.

No comments:

Post a Comment