KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, June 3, 2011

Miroslav Klose AKARIBIA KUONDOKA ALIANZE ARENA.


Mshambuliaji hatari wa kijerumani Miroslav Klose yu njiani kuachana na klabu yake ya sasa ya Bayern Munich kufuatia mazungumzo ya kuongeza mkataba wa kuendelea kuwepo klabuni hapo kutoonyesha dalili za mfanikio.

Miroslav Klose yu njiani kuondoka huku akihushwa na taarifa za kutaka kuelekea nchini Uturuiki kujiunga na klabu ya Trabzonspor, inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini humo na taarifa nyingine zikieleza kwamba huenda akajiunga na klabu ya Lazio ya nchini Italia.

Kwa kipindi cha majuma kadhaa sasa Miroslav Klose amekua katika mazungumzo na uongozi wa klabu ya Bayern Munich, ambao upo tayari kumpa mkataba wa mwaka mmoja hatua ambayo anaipinga na kushurutisha apewe mkataba wa kuanzia miaka miwili ama zaidi.

Nchini Uturuki tayari raisi wa klabu ya Trabzonspor, Sadri Sener ameshajinasibu mbele ya vyombo vya habari kwa kuahidi kumsajili mshambuliaji huyo kwa ajili ya msimu ujao huku akimini uwezo wa kumpata upo kama alivyopanga.

Amesema sifa kubwa waliyonayo ya kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32 ni ushiriki wao katika michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya msimu ujao sambamba na mafanikio yaliopo ndani ya klabu hiyo.

Katika msimu wa mwaka 2010-11 Miroslav Klose alifanikiwa kupachika mabao 20 na kwa ujumla toka alipoanza kuitumikia klabu hiyo ya Alianze Arena amechafunga mabao 61 katika michezo 109 aliyocheza.

Wakati Miroslav Klose akiwa mbioni kuondoka Alianze Arena, uongozi wa klabu ya Bayern Munich imetangaza kuingia kwenye heka heka za kutaka kumsajili mshambuliaji wa pembeni wa klabu bingwa nchini Ufaransa Lille Eden Hazard.

Bayern Munich wametangaza dhamira hiyo huku wakikaribia kumsajili kipa wa klabu ya Schalke 04 Manuel Neuer, Nils Petersen pamoja na Márcio Rafael Ferreira de Souza.

No comments:

Post a Comment