KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, June 9, 2011

Miroslav Klose HUYOOOOOOOOOO STADIO OLYMPICO.


Siku mbili baada ya kufunguliwa mlango huko Allianze Arena yalipo makao makuu ya klabu ya Bayern Munich, mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Ujerumani Miroslav Klose amekamilisha usajili wa kuichezea klabu ya SS Lazio ya nchini Italia.

Miroslav Klose amejiunga na klabu hiyo ya Stadio Olympico akiwa kama cmchezaji huru na amesaini mkataba wa miaka miwili ambao utafikia kikomo mwezi June mwaka 2013.

Raisi wa klabu ya SS Lazio Claudio Lotito ametangaza hatua hiyo kupitia mtandao wa klabu yake ambapo amesema ni faraja kubwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji muhimu pamoja na mashuhuri ulimwenguni ambapo wanaamini atawasaidia katika mipango yao ya msimu ujao wa ligi.

Amesema ilikua ni kazi ngumu kumshawishi Klose kujiunga nao hasa ikizingatiwa vilabu kadhaa vya barani ulaya vilitamani kumpata baada ya kusikia sakata lake na uongozi wa klabu ya Bayern Munich lakini bahati imeangukia kwao na katu hawatoichezea.

Vilabu vilivyokua tayari kumsajili Miroslav Klose ni Everton ya nchini Uingereza, Valencia ya nchini Hispania, Trabzonspor pamoja na Galatasaray zote za nchini Uturuki.

Miroslav Klose mwenye umri wa miaka 33, ameondoka nchini kwoa Ujerumani kufuatia kushindwa kufikia muafaka na uongozi wa klabu ya Bayern Munich ambao ulitamani kumpa mkataba wa mwaka mmoja ili hali yeye binafsi alihitaji mkataba wa miaka miwili baada ya mkataba wa awali kufikia kikomo mwishoni mwa msimu wa mwaka 2010-11.

No comments:

Post a Comment