KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, June 3, 2011

MISUKOSUKO YA KISIASA IMETUSAIDIA.


Wakati mataifa ya barani Afrika kesho yakitarajia kurejea kwenye vita ya kuwani nafasi 14 za kucheza fainali za mataifa ya bara hilo, kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tunisia Sami Trabelsi amesema anaamini mapinduzi ya kisiasa yamesaidia kupatikana na mwenendo mzuri wa mchezo wa soka nchini humo.

Sami Trabelsi ambae atakishuhudia kikosi chake kikirejea uwanjani juma hili kucheza na timu tya taifa ya Chard katika mchezo wa kundi K, amesema utaratibu wa maendeleo ya soka nchini humo kwa sasa umekua na tofauti kubwa ambayo inamfanya kila mmoja wao kujituma.

Amesema bado wana kazi ya kufanya katika michezo ya kundi K lakini anaamini kikosi chake kilichosheheni wachezaji wengi wanaosukuma soka la nyumbani kitafanya vyema hasa ikizingatia walijitahidi kucheza kwa kujituma zaidi na kutwaa ubingwa wa fainali za mataifa bingwa barani Afrika zilizofanyika nchini Susdan mapema mwaka huu.

Sami Trabelsi aliekiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Tunisia katika fainali za kombe la dunia za mwaka 1998 kule nchini Ufaransa pia amekiri kukosekana kwa michezo ya ligi baada ya mapinduzi ya kisasa napo kulisaidia kwa kila mchezaji kujitemngenezea mazingira mapya ya kucheza soka katika mfumo tofauti mara baada ya aliekua raisi wa nchi hiyo Zine al-Abidine Ben Ali kuondoka madarakani.

Timu ya taifa ya Tunisia inakamata nafasi ya tatu kwenye kundi K kwa kufikisha point saba nyuma ya timu ya taifa ya Malawi yenye point 9 huku timu ya taifa ya Botswana ikiwa tayari imeshafuzu kucheza fainali za Afrika kufautia kujizolea point 16.

No comments:

Post a Comment