KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, June 9, 2011

MKUTANO WA KUSAKA MUAFAKA KUFANYIKA ALLIANZE ARENA.Uongozi wa klabu ya Bayern Munich umeomba kufanya kikao cha mazungumzo ya kutafuta amani dhidi ya mashabiki wa klabu hiyo ambao wanapinga mipango iliyotangazwa kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Mtendaji mkuu wa klabu ya Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amesema ombi hilo kwa mashabiki tayari limeshawasilishwa kwa wahusika na wanategemea kukutana july 2 katika ukumbi wa mikutano wa Allianze Arena.


Amesema kikao hicho kitawahusishwa viongozi wa klabu pamoja na wawakilishi kumi wa uomoja wa mashabiki ujulikanao kama The Bavarians na wanaamini muafaka utapatikana kama wanavyotarajia.

Kwa muda sasa The Bavarians wamekua wakimpinga raisi wa klabu ya Bayern Munich Uli Hoeness kufuatia mpango wake wa kumsajili kipa wa klabu ya Schalke 04 Manuel Neuer ambae inadaiwa hawavutii mashabiki hao kwa itikadi binafsi.

No comments:

Post a Comment