KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, June 7, 2011

NASIKITISHWA NA TAARIFA HIZI - Massimo Moratti.


Raisi wa klabu bingwa duniani Inter Milan Massimo Moratti amekanusha taarifa za klabu hiyo kuwa mbioni kumsajili kiungo wa kimataifa toka nchini Brazil pamoja na klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania Ricardo Izecson dos Santos Leite Kaka kwa makubaliano ya kubadilishana na beki wa pembeni Maicon Douglas Sisenando.

Massimo Moratti amekanusha taarifa hizo wakati wa mahojiano na mwandishi wa gazeti la michezo la kila siku nchini Italiwa liitwalo Gazzetta dello Sport ambapo amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote na amekua akishangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuripoti uvumi huo.

Raisi huyo wa Inter Milan amesema kwa sasa ajihisi mwenye furaha kufuatia taarifa hizo za uzushi ambapo amekua akipata maswali kila kona ya mji wa Milan anayopita kuhusiana na suala hilo.
Hata hivyo inadaiwa kwamba meneja wa klabu ya Real Madrid José Mário dos Santos Félix Mourinho amekua katika mipango ya kutaka kumsajili beki wa pembeni wa inter Milan Maicon Douglas Sisenando kwa namna yoyote ile hatua ambayo inafananishwa na fununu zilizopo za kutaka kubadilishana kwa kumtoa Ricardo Izecson dos Santos Leite Kaka.

No comments:

Post a Comment