KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, June 10, 2011

NYOTA YA Vincenzo Montella YAENDELEA KUNG'AA.


Aliekua meneja wa muda wa klabu ya AS Roma Vincenzo Montella ametangazwa kuwa meneja wa klabu ya Catania inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini humo *SIRIE A*.

Vincenzo Montella ametangazwa kushika wadhifa huyo huko Stadio Angelo Massimino, baada ya kuondoka kwa Diego Simeone aliekua meneja wa kikosi cha klabu hiyo msimu uliopita.

Uongozi wa klabu ya Catania umemtangaza Montella kushika nafasi ya umeneja huku ukiamini mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Italia pamoja na klabu za Empoli , Genoa , Sampdoria , Roma na Fulham ataweza kurekebisha makosa yaliyojitokeza msimu uliopita.

Hata hivyo asubuhi hii uongozi wa klabu ya Catania unatarajia kumtambulisha Vincenzo Montella kwa waandishi wa habari ambapo pia utaeleza mipango yao kwa ajili ya msimu mpya wa ligi.

Meneja aliondoka klabuni hapo juma lililopita Diego Simeone alijitahidi kwa uwezo wake wote msimu wa mwaka 2010-11 hatua ambayo ilimsaidia kukifikiksha kikosi cha Catania katika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi ya Sirie A.

No comments:

Post a Comment