KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, June 14, 2011

Raymond Domenech AWINDWA ALGERIA.


Wakala wa aliekua kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ufaransa Raymond Domenech amesema mamlaka ya soka nchini Algeria ipo katika harakati za kumshawishi mtu wake ili aweze kukubali kukinoa kikosi cha nchi hiyo ambacho kwa sasa kipo kwenye kampeni za kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Afrika za mwakwa 2012.

Laminak Conseil, wakala wa kocha huyo aliekiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa katika fainali za kombe la dunia za mwaka 2010, huko nchini Afrika kusini amesema pamekuwepo na vishawishi vya kila aina kutoka nchini Algeria lakini bado maamuzi yapo kwa Domenech mwenyewe.

Hata hivyo wakala huyo amesema pamoja na kuwepo kwa vishawishi hivyo tayari kocha huyo mwenye umri wa miaka 59 amelazimika kutuma maombi kufutia uwezekano wa kupatikana kwa kazi hiyo kuwepo kwa asilimia mia moja.

Hata hivyo Raymond Domenech atakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ivory Coast Vahid Halilhozdic ambae tayari ameshawasilisha barua ya maombi ya kazi.

Argeria wapo katika mchakato wa kusaka kocha wa timu ya taifa kufuatia kujiuzulu kwa kocha mzawa Abdelhak Benchikha baada ya kupokea kisago cha mabao manne kwa sifuri kilichotolewa na timu ya taifa ya Morocco majuma mawili yaliyopita.

Katika kampeni za kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya bara la Afrika timu ya taifa ya Algeria imepangwa katika kundi D sambamba na timu ya taifa ya Tanzania, Jamuhuri ya Afrika ya kati pamoja na Morocco.

No comments:

Post a Comment