KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, June 10, 2011

REAL MADRID WAPINGA ADHABU YA MOURINHO.


Uongozi wa klabu ya Real Madrid umekata rufaa katika shirikisho la soka barani Ulaya UEFA ya kupinga adhabu ya kufungiwa michezo mitano iliyo chini ya shirikisho hilo iliyomuangukiwa Jose Mourinho.

Real Madrid wamefanya jitihada hizo huku ikiwa tayari Jose Mourinho akiwa katika fikra za kutaka kuipeleka kesi hiyo katika mahakama ya kimichezo CAS kwa madaia ameonewa na kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka barani Ulaya.

Tayari UEFA wamethibitisha kupokelewa kwa rufaa hiyo ya Real Madrid na wakati wowote kuanzia juma lijalo itasikilizwa huku viongozi wa klabu hiyo ya Estadio Stantiago Bernabeu wakiamini kamati ya rufaa itampunguzia adhabu Mourinho.

UEFA walifikia hatua ya kumfungia Jose Mourinho michezo mitano kufautia matatizo yaliyojitokeza katika mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu wa mwaka 2010-11 ambapo meneja huyo alimpinga muamuzi Wolfgang Stark kutoka nchini Ujerumani baada ya kumuonyesha kadi nyekundu Pepe ambae alidaiwa kumchezea ovyo beki wa kulia wa FC Barcelona Daniel Alves.

Kufautia kitendo hicho muamuzi alimuadhibu Mourinho kwa kumtaka aondeke katika benchi la Real Madrid hatua ambayo ilipelekea meneja huyo wa kireno kuketi pamoja na mashabiki jukwaani.

Hata hivyo mara baada ya mchezo huo kumalizika ambapo Real Madrid walipokea kisago cha mabao mawili kwa sifuri, Jose Mourinho alizungumza kwa hasira mbele ya waandishi wa habari huku akiwakashifu wapinzani wake kwa kusema wanabebwa na pengine0 hatua hiyo inasababishwa na udhamini wa shirika la kuwahudumia watoto duniani UNICEF.

Pia akamkashifu meneja wa klabu ya Barcelona Josep Pep Guardiola Isala kwa kusema ni meneja ambae amekua akifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ulaya kwa kashfa ambapo alichukulia mfano wa mwaka 2009 walipotawazwa kuwa mabingwa wa michuano ya Ulaya baada ya kuifunga Man utd huku katika hatua ya nusu fainali wakiifunga Chelsea mchezo ambao uliacha malalamiko kwa muamuzi.

Mourinho hakuishia hapo akaongeza kwamba endapo Guardiola angepata ubingwa wa ulaya msimu wa mwaka 2010-11 hatua ambayo imekua kweli, bado atakua katika kasha ya kikosi chake kubebwa kutokana na utaratibu mbovu wa uchezeshaji uliojitokeza huko Estadio Stantiago Bernabeu.

No comments:

Post a Comment