KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, June 9, 2011

Roberto Martinez APEWA SAA 24 ZA KUFANYA MAAMUZI.


Mwenyekiti wa klabu ya Wigan Athletic Dave Whelan anatarajia kupata jibu kamili la meneja wa klabu hiyo Roberto Martinez ambae kwa siku ya hii leo amekua akihusishwa na taarifa za kutaka kujiunga na klabu ya Aston Villa.

Dave Whelan anatarajia kupata jibu hilo ndani ya saa 24 zijazo huku akiamini kwamba Roberto Martinez bado ana mapenzi ya dhati na klabu ya Wigan na huenda hatua hiyo ikapelekea kubaki huko DW Stadium kama mkataba wake unavyoelekeza.

Mwenyekiti huyo wa klabu ya Wigan amefanya maamzi ya kumpa Roberto Martinez muda wa kufikiri baada ya kumuwashia taa za kijani kwa ajili ya kuondoka klabuni hapo endapo atahitaji kufanya hivyo kutokana na safari iliopo ya kusaka maisha yake.

Akizungumza na shirika la utangazaji la nchini Uingereza BBC Dave Whelan amesema maamuzi ya kumpa muda Martinez pia yamezingatia mazungumzo yao yaliyochukua nafasi usiku wa kuamkia hii leo ambapo walizungumza mengi kwa ajili ya mustakabali wa kimaisha pamoja na wa klabu.



Katika msimu wa mwaka 2010-11 Roberto Martinez alifanya kazi kubwa ya kukinusuru kikosi chake kusalia katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza kufuatia hali kumuendea kombo hadi katika mchezo wa mwisho dhidi ya Stoke City ambapo alihitajika kupata ushindi, hatua ambayo ilitimia kufuatia bao lililofungwa na Hugo Rodarega.

Mara baada ya mchezo huo akiwa na furaha isiyo na kifani Roberto Martinez alikipongeza kikosi chake kwa kazi nzuri iliyofanywa na pia akajisifia yeye binafsi kwa ujasiri aliokua nao wakati wote wa msimu.

Hata hivyo katika kinyan’ganyoro cha kuwania nafasi ya umeneja wa klabu ya Aston Villa Roberto Martinez hayupo pekee yake kufuatia jina la meneja wa klabu ya Bolton Wanderers Owen Coyle kutajwa kila kona huko mjini Birmingham.

Klabu ya Aston Villa kwa sasa haina meneja wa kukiongoza kikosi cha klabu hiyo kufuatia kuondoka kwa Gerard Houllier majuma mawili yaliyopita.

No comments:

Post a Comment