KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, June 2, 2011

Ruud van Nistelrooy ARUDI HISPANIA.


Mshambuliaji wa kidachi Ruud van Nistelrooy amewasili mjini Malaga tayari kwa utaratibu wa kusiani mkataba wa mwaka mmoja na viongozi wa klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini humo.

Van Nistelrooy, mwenye umri wa miaka 35, amewasili mjini humo siku mbili zilizopita kwa usafiri wa ndege binafsi akitokea nchini kwao Uholanzi ambapo imeelezwa kwamba wakati wowote kuanzia hii leo atakamilisha dili la kujiunga na klabu ya Malaga inayomilikiwa na mfanyabiashara wa kimataifa toka nchini Qatari Abdullah Ghubn.

Uongozi wa klabu ya Malaga umevutiwa na Ruud van Nistelrooy kufuatia uwezo wake wa upachikaji mabao anapokua uwanjani huku ikiaminiwa usajili wake utaamsha ari kwa wachezaji wengine huko Estadio La Rosaleda.

Ruud van Nistelrooy yu mbioni kujiunga na klabu hiyo akiwa kama mchezaji huru baada ya mkataba wake na klabu ya Hamburg ya nchini Ujerumani kufikia kikomo mwishoni mwa msimu uliopita.
Endapo mshambuliaji huyo atafanikisha utaratibu wa kusajiliwa na klabu ya Malaga atakua akirejea nchini Hispania kwa mara ya pili, ambapo kwa mara ya kwanza akiwa nchini humo aliitumikia Real Madrid toka mwaka 2006–2010 na alicheza michezo 68 na kufunga mabao 46.

Uongozi wa klabu ya Malaga pia unaendelea na utaratibu wa kutaka kumsajili kiungo mchezeshaji wa klabu ya Parlemo ya nchini Italia Javier Pastore.

Na taarifa tulizozipokea muda mchache uliopita zinaeleza kwamba Ruud van Nistelrooy tayari ameshakamilisha taratibu za kujiunga na klabu ay Malaga baada ya kusaini makataba wa mwaka mmoja.

No comments:

Post a Comment