KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, June 6, 2011

SAMIR NASRI AWAWEKA ROHU JUU WANA ARSENAL.


Kiungo wa kimataifa toka ncdhini Ufaransa pamoja na klabu ya Arsenal Samir Nasri ameendelea kuongeza mashaka ya kuihama klabu hiyo ya jijini London baada ya kugoma kusaini mkataba mpya na uongozi wa The Gunners.

Samir Nasri ambae kwa sasa yupo na timu ya taifa ya Ufaransa inayosaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Ulaya za mwaka 2012, ameongeza mashaka hayo kufuatia kauli aliyoitoa wakati wa mahojiano na televisheni ya TF1 ambapo amesema bado hajafahamu kama ataendelea kuwepo Arsenal ama la, lakini anachojua kwa sasa mazungumzo na kumtaka asini mkataba mwingine yanaendelea.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, alipoulizwa juu ya uvumi wa kutaka kuhamia kwa mabingwa wa soka nchini Uingereza Man utd, hakua tayari kujibu swali hilo moja kwa moja zaidi ya kumueleza muandishi wa habari wa kituo hicho cha televisheni kuwa na subra na kuona kama ataendelea kuwa mshika bunduki msimu ujao.

Siku kadhaa zilizopita beki wa pembeni wa klabu ya Man Utd pamoja na timu ya taifa ya Ufaransa Patrice Evra alitoa kauli ya kumshawishi Samir Nasri kwa kumtaka abadili klabu na kujiunga nae huko Old Trafford endapo anahitaji kushinda mataji.

Mkataba wa Samir Nasri huko Emirates umesaliwa na mwaka mmoja na endapo ataendelea kugoma kusaini mkataba mpya huenda uongozi wa Arsenal ukamuuza kwa kuhofia kumuachia kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu ujao.

No comments:

Post a Comment